MAJUKUMU YA MHASIBU MKUU WA SERIKALI

  1. Kumsaidia Katibu Mkuu ambaye ni Mlipaji Mkuu wa Serikali katika mambo yote ya usimamizi wa Fedha za Mapato na Matumizi Serikalini.
  2. Kumsaidia Katibu Mkuu ambae ni Mlipaji Mkuu wa Serikali katika usimamizi wa matumizi ya Mfuko Mkuu wa Serikali.
  3. Kusimamia ukusanyaji wa mapato na udhibiti wa fedha na rasilimali za Serikali katika Wizara /Idara / Taasisi Serikalini.
  4. Kutoa Maelekezo, Miongozo na Maagizo kwa Taasisi za Serikali kuhusiana na uwasilishaji wa Hesabu za mwaka na ripoti zinazohusika.
  5. Kusimamia Wizara/Idara za Serikali katika ufungaji wa Mahesabu kwa kiwango kinacho kubalika Kimataifa.
  6. Kusimamia Mfumo wa kazi za Kihasibu Serikalini na kuona zinatekelezwa ipasavyo kwa kufuata Sheria, Kanuni, taratibu, miongozo na maelekezo yanayo husina na utekelezaji wa kazi hizo.
  7. Kusimamia mambo yote ya Fedha, Hesabu za Benki za aina zote zilizo chini ya uangalizi wa Serikali na kwamba zinafanyiwa ukaguzi kwa mujibu wa Sheria na Kanuni zake.
  8. Kuwasilisha kwa Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesbu za Serikali taarifa mbalimbali, ripoti za Jumuisho la Hesabu za Serikali zilizofungwa ambazo zinaonyesha hali halisi ya mali za Serikali ziliopo na Madeni inayodaiwa.
  9. Kusimamia Sheria ya Usimamizi wa Fedha za Umma na kufanya mapitio ya Miongozo mbalimbali ya fedha Nchini na ya Kimataifa kwa kuzingatia hali halisi iliyopo na ijayo.
  10. Kusimamia Deni la Taifa na kutoa miongozo kwa Wizara/ Idara /Taasisi za Serikalini.

Zanzibar