1.    MIRADI ILIYOPO CHINI YA IDARA YA MITAJI YA UMMA

       Idara ya Mitaji ya Umma inasimamia Miradi ya Serikali ifuatayo:

 1. Programu ya Ujenzi wa Afisi za Serikali – Unguja.
 1. Ujenzi wa jengo la Ofisi ya Wizara ya Nchi Afisi ya Rais, Katiba, Sheria na Utawala Bora- Mazizini(Ujenzi huu tayari umekamilika).
 2. Uendelezaji wa jengo la Ofisi ya Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, wanawake na Watoto - Mwanakwerekwe.
 3. Ujenzi wa Chuo cha Uandishi wa Habari – Kilimani(Mradi wa Ujenzi huu umekamilika).
 4. Ujenzi wa Chumba cha Kuhifadhia Maiti kwa ajili ya Mafunzo ya Vitendo katika chuo Kikuu cha Taifa – SUZA (Ujenzi huo upo katika hatua za awali).

     2.  Programu ya Ujenzi unaoendelea wa Majengo Matatu (3) ya Ofisi za Serikali – Pemba.

 1. Ujenzi wa Ofisi ya Wizara ya Fedha  na Mipango.
 2. Ujenzi wa Ofisi Wizara ya Nchi Afisi ya Rais, Katiba, Sheria na Utawala bora.
 3. Ujenzi wa Ofisi Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Vijana, wanawake na Watoto.

     3.  Mradi wa Mageuzi katika Usimamizi wa Fedha (PFMRP).

 1. Kufanya mapitio ya Sheria ya Mitaji ya Umma.
 2. Kuandaa Sera ya Usimamizi wa Mali za Serikali (Public Asset Management Policy).
 3. Kusimamia Daftari la Kumbukumbu la Mali za Serikali(Asset Register).

 

2.    MAJUKUMU NA KAZI ZA IDARA YA MITAJI YA UMMA

       Idara hii imegawika katika Divisheni kuu mbili kama ifuatavyo:-

 1. DIVISHENI YA MITAJI YA UMMA
 1. Kusimamia Mashirika ya Umma, Mitaji ya Umma pamoja na Hisa za serikali katika Kampuni Binafsi kama ilivyoelekezwa katika Sheria ya Mitaji ya Umma No 4. 2002.
 2. Kufanya tathmini juu ya utendaji wa Mashirika ya Umma na Usimamizi wa hisa.
 3. Kuhakikisha utekelezajiwa sera za Serikali katika  kuyaimarisha Mashirika ya Umma.
 4. Kuimarisha sera, taratibu na miongoza ya utekelezaji katika kuyafanyia mageuzi Mashirika ya Umma.
 5. Kuzifanyia mapitio Sera, Sheria na Miongozo na kuandaa mapendekezo ya kuziimarisha.
 6. Kuandaa na kutoa miongozo itakaopelekea kuzingatiwa na kutekelezwa wa maamuzi na maagizo ya Serikali.
 7. Kusajili mashirika ya Serikali pamoja na kutunza daftari la usajili.
 8. Kufanya tathmini kwa miradi mipya inayotekelezwa kwa miradi iliyoanzishwa na Mashirika ya Umma.
 9. Kuishauri Serikali juu ya kuanzisha, kuunganisha au kuvunja shirika la Serikali.
 10. Kuishauri Serikali namna ya kuingia ubia na mwekezaji au shirika binafsi.
 11. Kufuatilia mikataba ya makubaliano ya mikopo baina ya Serikali katika Mashirika ya Umma.
 12. Kumiliki kwa niaba ya Serikali uwekezaji, mitaji pamoja na hisa.
 13. Kuchambua na kuandaa mapendekezo  juu ya mipango ya muda mrefu na mfupi ya mashirika ya umma na kuioanisha na mipango ya uchumi wa nchi.
 14. Kufanya jambo jengine lolote litakalofanikisha kufikiwa malengo ya Idara.

Zanzibar